Ni kawaida kwa watu kuficha na wakati mwingine kudanganya umri wao pengine kwa kuhofia kuonekana ama wadogo sana au wakubwa zaidi katika kundi la watu.
Utafiti uliofanywa unadai unaweza kuendelea kuuficha umri wako na kuwadanganya watu kwa sababu itakusaidia kuishi zaidi.
Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa watu wanaoamini kuwa ni wadogo kiumri tofauti na kilichopo katika vyeti vyao vya kuzaliwa ni miongoni mwa kundi la watu wenye uwiano mdogo wa kufa ukilinganisha na ama wanaouhisi umri wao au wanaojifaya wakubwa kuliko umri wao .
Utafiti umechapishwa na JAMA INTERNAL MEDICINE ONLINE ambao ulikusanya data kutoka kwa watu 6,489 wenye wastani wa miaka 65.8 ambao wanaelezwa kujihisi watoto wa chini ya umri wa miaka 10.
Kinachofurahisha zaidi ni kuwa watu wengi kwenye utafiti huo hawakuwa na hisia na umri wao halisi ambapo wengi walidai kujihisi kama watoto wa miaka mitatu huku 4.8% walikuwa wanajihisi wakubwa zaidi ya umri wao.
0 comments:
Post a Comment