Mahakama kuu nchini Uingereza imepitisha maombi ya ligi kuu ya Uingereza ya kuzuia mbinu za kutizama soka kuitia vyanzo vya Intaneti kwa mfumo maarufu wa Kodi set-top boxes.
Amri ya mahakama inamaanisha kuwa ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Premier League kwa sasa inaweza kuzuia vyanzo vya kompyuta ambavyo huzipa nguvu njia za kutizama matangazo ya soka kwa njia zisizokuwa halali.
Msemaji alisema: Kwa mara ya kwanza ligi kuu ya Uingereza itaweza kuvuruga na kuzuia njia zisizo halali kupitia intaneti ambazo hutumika kupitia vyanzo vya IPTV, au kwa jina lingine Kodi, boxes.
“Hii itatusaidia kuwatambua wasambazi wa njia hizi zisizokuwa halali kwenda kwa IPTV boxes, na pia intaneti katika njia nzuri na salama.”
Haki za matangazo kwa msimu wa mwaka 2016-19 ziliuzwa kwa thamani ya takribani paundi bilioni 5.16 mwaka 2015.
Msemaji wa kampuni ya kurusha matangazo ya Sky alisema: “tumefurahishwa na maamuzi ya ligi kuu ya Uingereza kuamua kupiga chini njia hizi ambazo hutumika kutizama soka. Kuingilia maudhui na kudukua ni wizi na kufanikiwa kwa maombi haya ni mwanzo mzuri wa kupambana na hili tatizo.
“Tutaendelea kufanya kazi na wenye haki miliki, serikali, masoko ya njia za mtandao na watengeneza maudhui katika kupambana na udukuzi huu wa kisasa na kuwafanya watu kutambua athari za udukuzi huu ambazo wanaweza kukutana nazo.”
0 comments:
Post a Comment