255 Champion Boy Mbwana Samatta kafanya yake kwenye usiku wa Ulaya wakati klabu yakeya KRC Genk ikicheza mchezo wa kwanza wa 16 bora wa michuano ya Europa League dhidi ya Gent.
Samatta akiwa katika kiwango cha juu ameweka kambani bao mbili katika mchezo huo uliomalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 ugenini dhidi ya Gent ambao ni wapinzani wao kutoka kwenye ligi kuu ya Ubelgiji.
Malinovsky alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa mkwaju mkali wa free-kick nje ya box ambao aliukandamiza kwa mguu wake wa kushoto na kutinga moja kwa moja wavuni. Samuel Kalu akaisawazishia Gent dakika ya 27.
Dakika ya 33 Omary Colley akaifungia Genk bao la pili akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa kwa mguu wa kushoto na Malinovsky.
Golden Boy Mbwana Samatta akafunga goli lake la kwanza kwenye mchezo huo huku likiwa ni goli la tatu kwa timu yake dakika ya 41 akipokea pasi ya Boetius kwa kuuweka mpira kifuani kisha kuachia bakora kali kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya penati box.
Genk ikaendelea kupambana kutafuta ushindi mkubwa wa ugenini na hatimaye malengo yao yakaendelea kufanikiwa baada ya Jere Uronen kufunga goli la nne akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Pozuelo dakika ya 45 kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa Gent kuandika bao lao la pili lililofungwa na Kalifa Coulibaly dakika ya 61 huku Jeremy Perbet akipoteza nafasi ya kuifungia Gent bao la tatu kwa mkwaju wa penati.
Dakika ya 72 nahodha wa Tanzania akaweka kambani bao lake la pili kwenye mchezo huo huku likiwa ni bao la tano kwa Genk akiitendea haki pasi ya mwisho ya Thomas Buffel akiwa ndani ya sita na kuiweka timu yake kwenye mazingira mazuri ya kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Europa League.
Matokeo ya ushindi wa magoli 5-2 waliopata Genk wakiwa ugenini, yanawaweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele na kucheza hatua inayofata (robo fainali ya Europa League) kwani Gent watahitaji ushindi wa magoli 4-0 iki kuitoa Genk kwenye mchezo wa marudiano ambapo Genk watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumani.
0 comments:
Post a Comment