Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh Josephat Sinkamba amewataka watendaji wa Halmashauri kuwa wabunifu ukiwemo wa kutumia rasilimali ya takataka kuwa fursa ya kuzalisha nishati ya gesi na umeme hatua ambayo licha ya kusaidia kudumisha usafi itaongeza ajira na kuwarahisishia wananchi maisha.
Hata hivyo Naibu Waziri amewapongeza watendaji wa jiji la Arusha kwa kuanza mchakato wa kutumia takataka kuzalisha umeme na amewataka kuharakisha utekelezaji wake ili iwe mfano na chachu kwa halmashauri zingine.
0 comments:
Post a Comment