Michel Jackson alizaliwa tarehe 29 August mwaka 1958, akiwa ni mtoto wa nane kati ya kumi wa mzee Joe Jackson na Catherine Jackson, alikuwa na madada wa 3 ambao ni Rebbie, La Toya na Janet, huku makaka zake ni Jackie, Tito, Jermaine, Marlon, Randy, na ndugu yake mwingine anayeitwa Brandon alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Alianza kuimba akiwa umri wa miaka mitano akiwa na kundi la Jackson 5, kundi lakifamilia kwani waimbaji wote katika kundi hilo walikuwa ni ndugu zake wa damu, kundi hilo lilifanya vizuri sana nchini marekani na dunia nzima kwa ujumla.
Jackson hakuwa na mahusiano mazuri na baba yake Joe Joseph Jackson aliwahi kusema kuwa alikuwa na kawaida ya kumchapa Michael wakati akiwa mtoto, na Michael aliwahi kulalamika kuwa baba yake alikuwa akimnyanyasa kwa kumpiga hasa wakati wa Rehalse ingawa aliwahi kukiri kuwa baba yake alichangia kwa kiasi kikubwa yeye kupata mafanikio.
1968 Boby Taylor na The Vancouver waliligundua Kundi la Jackson 5 ambapo kundi hilo likasign na Motown Records na walifanikiwa kurekodi ngoma zilizotisha enzi hizo kama ABC, I want u Back, I’ll be there na nyinginezo, walirekodi album 14 na Motown na Michael alirekodi album nne za solo.
Jackson 5 walikaa na Motown mpaka ilipofika mwaka 1976 ambapo walidai wanataka uhuru wa kisanii na baada ya hapo wakaenda kusign na Epic, na kundi hilo lilibadilisha jina kutoka the Jackson 5 na kujiita The Jacksons na walirekodi album 6 kutoka 1976 mpaka 1984
1977 Michael alikutana na mtaarishaji wa muziki maarufu enzi hizo Quincy Jones chini ya Epic Records akarekodi album inayoitwa OFF THE WALL, ambayo ilifanya vizuri sana katika chart za nchi marekani.
1982 Wacko Jacko alirelease album ambayo inasemekana ni album ambayo imeuza sana kuliko album yoyote duniani, inaitwa THRILLER, ndani ya album hii kulikuwa na Single 7 ambaao zilihit sana dunia nzima, album hii iliuza copy milioni 50 dunia nzima, alifanya kazi na the best Producers na Directors na kufanikiwa kutengeneza Music video ya Thriller ambayo mpaka leo budget ya kutengeneza music video hiyo haijawahi kuvunjwa na msanii yeyote duniani.
1984 Wacko Jacko akavunja rekodi kwa kutunukiwa tuzo 8 za grammy ndani ya usiku mmoja, tuzo hizo zilitokana na Album yake ya Thriller na kitabu cha “T story book.”
Tarehe 9 December 1984 katika concert ya mwisho ya Jackson 5 iliyoitwa Jackson Victory Tour, Wacko Jacko akatangaza kuwa anajitoa kutoka kundi hilo na atakuwa anafanya kazi zake binafsi,
1987 Michael Jackson akarelease album yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake album inaitwa BAD na kuvunja rekodi ya Tour za msanii mmoja mmoja yaani Solo, kwani show zake zilikuwa zikihudhuriwa na malaki ya watu kila nchi aliyokanyaga..
1988 MJ kwa mara ya kwanza aliandika Autobiography yaani kitabu ambacho alizungumzia maisha yake kutoka utotoni na kazi yake ya muziki, Autobiography hiyo iliitwa MOON WALK.
Mwishoni mwa miaka ya 80 Mj alitajwa kama msanii wa Decade kutokana na mafanikio aliyoyapata katika Album zake za Thriller na Bad.
1991 MJ alisign mkataba na kampuni ya Sony Music, ambapo inasemekana ni mkataba mkubwa kuwahi kusainiwa na wanamuziki enzi hizo, MJ akatoa album yake ya nne Dangerous,
1992 akaanza kupiga Tour tena, na safari hii akazungukia nchi ambazo hazikuwahi kutembelewa na mwanamuziki yeyote wa POP na Rock , ambapo pia aliunda foundation ya kusaidia watoto maskini dunia nzima, iliitwa HEAL THE WORLD FOUNDATION, safari hii alifika mpaka nchini Tanzania kama mnakumbuka jamaa alifikia katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam.
1994 MJ alimwoa LISA MARIE PRESLEY. Mtoto wa Elvis Presly, na ndoa yao ilidumu kwa miezi 19 tu na kutalikiana mwaka 1996
1995 MJ akarelease Double album ambayo aliita History, nusu ya Album hii ilikuwa ni ngoma mpya na nusu iliyobaki ilikuwa ni Greatest hits.
1996 alioa kwa mara ya pili na safari hii bahati ilimwangukia Debbie Rowe ambae alikuwa na nurse na walikutana na MJ katika Hospitali aliyokuwa akifanya kazi Debbie na inasemekana MJ alienda kutibiwa Ngozi. Pamoja walifanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Paris na Prince Michael.
1997 MJ alirelease remix album aliyoiita BLOOD ON THE DANCE FLOOR.
2001 MJ alisherehekea miaka 30 ya kufanya kazi kama Solo Artist na alipiga show jijini Newyork na wasanii kibao wa kizazi kipya ambao walirudia kuimba ngoma zake live, wasanii hao ni pamoja na Shaggy, Whitney Houston, Destinies Child, Usher Raymond na wengine kibao.
2001 MJ alitoa album nyingine INVICIBLE ndani yake kulikuwa na Single kama U ROCK MY WORLD, na CRY.
2003 MJ akaachia single mpya ONE MORE CHANCE.
2009 March MJ akatangaza Come back Tour ambayo ilitakiwa kupigwa 02 ARENA jijini London mwezi wa saba, ilipanga kupiga tour kwa siku 10 lakini wadau wakataka aongeze siku 50 za Tour, zaid ya Tiket laki saba na nusu ziliuzwa, na tiket zote hizo ziliuzwa dakika chache tu baada ya tangazo lake..
Tarehe 25 June 2009 mshumaa ukazimika ghafla kwa ugonjwa ambao kitaalamu unajulikana kama Cardiac Arrest, familia ya MJ ilitangaza kuwa the greatest Singer of all time amefariki dunia.
Tutakumbuka MJ kwa mchango wako ulioutoa kwa watu weusi dunia nzima, kwani baada yako kila mtu aliamini kuwa mtu mweusi anaweza kufanya chochote na kikapendwa dunia nzima bila kujalisha ni wa rangi gani.
(#Pichani: Michael Jackson akiwa na Mh Rais Ali Hassan Mwinyi, alipotembelea Tanzania).
0 comments:
Post a Comment