Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye pia ni mwanaharakati wa masuala ya vijana, Dkt. Hamis Kigwangalla ameshindwa kujizuia na kufunguka jinsi anavyomuhusudu mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.
Kigwangalla ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nzega, ametumia ukurasa wake wa twitter kutamka rasmi kuwa hajawahi kuwa shabiki wa Diamond, lakini kazi zake anazikubali hasa zile zilizokaa kimikakati ya biashara.
"Sikuwahi kuwa mshabiki wa Diamond Platnumz, japokuwa ni mwimbaji mzuri, ila nakubali sana kipaji chake kwenye 'biashara' ya muziki" Amesema Kigwangalla
Ametaja ngoma iliyomfanya aanze kumkubali tena Diamond, mbali na ile ya Mbagala, kuwa ni Marry You aliyoshirikiana na Ne-Yo kutoka nchini marekani.
"Zaidi ya nyimbo ya Diamond Platnumz Mbagala (ambayo naipenda mpaka kesho), na juzi hapa nyimbo za Ngololo, Salome, hii ya Marry You" Aliandika Kigwangalla.
0 comments:
Post a Comment