Muigizaji Aunty Ezekiel amemtetea mpenzi wake (Mose Iyobo) kwa kumfananisha na nyani msanii chipukizi anayefananishwa na mmoja wa wasanii kutoka WCB (Harmo Rappa) kwa kusema ni sawa kabisa na Mose hakufanya makosa
Hivi karibuni akiwa kwenye Kipindi cha KIKAANGONI cha Facebook EATV Aunty amesema kwamba watu walimnukuu vibaya Mose na kumhukumu moja kwa moja huku akiongeza kwamba hakuwa na nia mbaya.
“Sikuona shida yoyote Mose kumuita Harmorappa nyani kwa kuwa ni majina ambayo vijana wa kisasa wanajipa, mfano kama Nasibu anavyojiita Simba, asilimia kubwa ya watu hawakujua kwa nini alijiita hivyo, wangemuuliza kwa nini ameamua kumfananisha na nyani ndipo wangehukumu, yule si msanii? basi inawezekana Mose labda baada ya kusikiliza wimbo wake kaona kwenye kuimba ana kisauti kama cha nyani au labda anarukaruka kama kinyani, kwa hiyo ni sawa kumuita nyani" Amesema Aunty.
Aunty amesema alichokifanya Mose ni kumsaidia Harmorapa kujiita nyani na kwamba Mose alichokosea ni kumuita kabla yeye (Hamorapa) hajajiita mwenyewe.
Aidha Aunty amesema kwa upande wake hamkubali kabisa Harmorapa kwa kuwa analazimisha kujulikana na hana kipaji
"Yule mshikaji simkubali kabisa anatumia nguvu nyingi na sababu kutafuta kujulikana kiufupi hajajipanga, hana kipaji" Amesema Aunty hivi
0 comments:
Post a Comment