Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ametangaza kuwa muungano wake wa NASA
utaendesha kampeni nchi nzima kushinikiza kufanyika mageuzi katika tume ya uchaguzi, IEBC,
akiendelea kushikilia msimamo wake kwamba uchaguzi wa Agosti 8 uliompa ushindi Rais Uhuru
Kenyatta ulikuwa na udanganyifu. Amesema maafisa wa tume hiyo wanapaswa kuondolewa. Odinga
amesisitiza kuwa tume hiyo lazima ifanyiwe mageuzi kabla hajashiriki katika uchaguzi wa marudio, huku
Rais Kenyatta akisema tume hiyo haitakiwi kubadilishwa. Ingawa Mahakama ya Juu ya Kenya iligundua
kuwepo udanganyifu katika uchaguzi huo, haikuwaondoa maafisa wa tume hiyo kabla ya uchaguzi wa
marudio wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 17. Rais Kenyatta ameionya mahakama kutoingilia kati.

0 comments:
Post a Comment