Kimbunga Maria kilichopata nguvu na kufikia kiwango cha tano kimepiga kisiwa cha Caribbean cha Dominica kikiwa na upepo wa kasi ya kilomita 260 kwa saa.
Waziri mkuu Roosevelt Skerrit aliandika katika mtandao wa Facebook kuwa paa la nyumba yake limeng'olewa.
Alisema nyumba yake ilifurika maji na baadaye kusema kuwa alikuwa ameokolea.
Uwanja wa ndege wa Dominica na bandari vimefungwa.
Maria kinapitia njia ambayo kimbunga kama hicho wa jina Irma kilisababisha uharibifu wakati kikipitia eneo hilo mwezi huu.
Kisiwa kilicho karibu cha Martinique kiliwekwa katika tahadhari huku kingine cha Ufaransa cha Guadeloupe kiliwaamrisha watu kuondoka.
Baaadhi ya sehemu hizo bado zinarejea hali ya kawaida baada ya kupigwa na kimbunga Irma , ambacho ni kimbunga cha kiwango cha tano kilichosababisha vifo vya watu 37 na kusababisha hasara ya mabiliono ya dola.
Visiwa vinavyokumbwa na kimbunga Maria ni pamoja na visiwa vya Leeward vikiwemo Antigua na Barbuda.
ituo cha vimbunga cha Marekani (NHC) kiliongeza nguvu ya kimbunga hicho siku ya Jumatatu kutoka kiwango cha pili hadi kiwango cha nne na kisha kiwango cha tano ambacho ni kiwango cha juu zaidi.
Watabiri wa hali ya hewa walionya kuwa mvua kubwa inayosababishwa na kimbunga hicho inaweza kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo ya kutishia maisha.
0 comments:
Post a Comment