Jaji mkuu David Maraga wa Kenya amemshutumu inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet nchini humo kwa kukataa wito wa kuimarisha usalama wa majaji na mahakama na hivybasi kuwahatarisha.
Katika taarifa baada ya mkutano wa muda mrefu na wanachama wa tume ya huduma za mahakama, JSC, jaji mkuu Maraga amesema kuwa idara ya mahakama na majaji hatahivyo itaendelea kutoa huduma zake.
Amesema kuwa wako tayari kukabiliana na lolote lile kutetea katiba na sheria ya Kenya.
JSC imebaini kwamba inspekta jenerali wa plisi ambaye anafaa kutoa usalama kwa idara zote za serikali amekaidi wito ya kuchukua hatua , hivyobasi kuhatarisha maisha ya maafisa waidara ya mahakama, mali na walalamishi kwa hatari, alisema.
Jaji mkuu alisistiza kuwa idara ya mahakama ni kitengo huru cha serikali sawa na uongoza wa taifa na bunge.
- Mbunge awasilisha ombi la kuondolewa kwa jaji Maraga Kenya
- Jaji jasiri aliyebatilisha uchaguzi wa urais Kenya
- Rais Kenyatta: Ni haki yangu kuikosoa mahakama
Na iwapo viongozi wamechoka kuwa na idara ya mahakama iliyo thabiti na huru, alisema waitishe kura ya maamuzi na kufutilia mbali.
Amesema kuwa inauma kwamba idara ya mahakama na majaji hususana wale wa mahakama ya juu wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na kusababisha maandamano, yaliofanyika nje ya mahakama ya juu mjini Nairobi, Nyeri, Nakuru na Eldoret
Jaji maraga amesema kuwa maandamano yalikuwa na ghasia na yalilenga kuishinikiza idara ya mahakama na majaji fulani.
"Idara ya mahakama haijawahi kuziagiza idara nyengine za serikali kuhusu majukumu yao waliopewa na raia wa Kenya pamoja na katiba .Tunataka kusema kwamba sheria lazima ifuatwe kila mara.
0 comments:
Post a Comment