RC Makonda ameyasema haya Leo MACHI 8 kwenye ukurasa wake wa instagram Unknown March 08, 2017 News No comments Mkuu wa mkoa wa dar Mh. Paul Makonda ameyasema haya katika ukurasa wake wa instagram leo siku ya wanawake duniani.. Asilimia kubwa ya WANAWAKE ni aina ya watu waliokuza watoto wao katika mazingira magumu, mateso, machungu na kunyanyasika kwa hali ya juu mara nyingine, na walikubali kupitia hayo ili tu MTOTO ASIMAME na kuwa mtu atakaejitegemea na kutegemewa siku moja, LAKINI kuna kundi kubwa lililodhamiria kwa makusudi kabisa kuwarudisha nyuma kwenye mategemeo yao hayo, kundi lililopanga kwa makusudi kabisa kuangamiza vijana wao kwa ajili ya maslahi yao binafsi, kundi lisilojali kwa namna yoyote struggle za kina MAMA hawa katika kuwakuza watoto wao, kundi linalowaharibu huku wakiwa WANAJUA kabisa athari kwa TAMAA TU ya mali za haraka. Kundi la WAUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA. Siku ya leo tunapoadhimisha SIKU YA WANAWAKE DUNIANI napenda kuchukua fursa hii kuwahakikishia kina MAMA wote na wananchi wa mkoa wangu wa DAR ES SALAAM kuwa sitakubali watoto mliowabeba matumboni mwenu miezi tisa na kuwalea kwa tabu wafe kwa MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA. Naomba tuungane na Muheshimiwa Rais wetu Magufuli kuhakikisha tunashinda dhidi ya wauaji na wanyonyaji wanaofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya. Kama uliweza kumtunza tumboni miezi tisa basi usikubali mtoto wa mwingine akakatisha matumaini yako, mlinde mwanao ili ule matunda ya uzao wako.. A post shared by Paul Makonda (@paulmakonda) on Mar 8, 2017 at 3:11am PST Share This: Facebook Twitter Google+ Stumble Digg Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
0 comments:
Post a Comment